Sunday, April 8, 2012

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII YA LEO YA PASAKA!

Nimefufuka na ningali pamoja nawe; umeniwekea mkono wako, maarifa hayo ni ya ajabu.....aleluya!

Bwana amefufuka kweli kweli.....Aleluya! Utukufu na Ukuu una yeye hata milele na milele.

Ee Mungu, umetufungulia leo mlango wa milele kwa njia ya Mwanao wa pekee aliyeshinda mauti. Tunakuomba utujalie sisi tunaoadhimisha kufufuka kwake Bwana wetu, tufufuke katika nuru yako kwa kufanywa wapya na Roho wako.

Paska wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani Kristu; basi na tuifanye karamu kwa yasiyo chachika, ndio weupe wa moyo na kweli.......aleluya!!!!

No comments:

WATEMBELEAJI