Wednesday, May 23, 2012

MISELE KATIKA SEMINA YA MAJI DODOMA - VIJIJINI.

 Magari kama haya huwa nayaita Maboti au  Madungu, sijayazoea na siyapendi hata kuendesha, lakini inanibidi sasa kuendesha...mimi nimezoea ki punda changu Kisuzuki. Lakini yanasaidia sana kwa shughuli za vijijini, maana unapita sehemu ambazo huwezi amini, sehemu ngumu sana za Vijijini.
 Usafiri wa Ofisini CPPS - WATER PROJECT, wa kupigia misele ya hapa na pale Vijijini katika kuelimisha watu wa Vijijini kuhusu uchimbaji visima vya maji safi na salama, kutokana na shida ya maji iliyopo vijijini Dodoma.
 Kijiji cha Kisima cha Ndege - Dodoma Vijijini. Leo tukiwa na semina ya maji Kijijini hapa.
 Ofisi ya Mwenyekiti wa Kijiji hiki cha Kisima cha Ndege.

Kijijini Kisima cha Ndege - Dodoma Vijijini.

1 comment:

ray njau said...

Hongera sana Chibiliti kwa kumbuka kuwa kuwa na moyo kugawana kile kidogo pamoja nduguzo.
"KITAMU KULA NA NDUGU NA KICHUNGU KULA NA........."!
-----------------------------------
27 Usiwanyime watu mema wanayostahili, mkono wako ukiwa na uwezo wa kuyafanya. 28 Usimwambie mwenzako: “Nenda, kisha urudi na kesho nitakupa,” na kumbe una kitu anachohitaji. 29 Usimtungie mwenzako jambo lolote baya, wakati anapokaa nawe na kujiona salama. 30 Usigombane na mtu bila sababu, ikiwa hajakufanyia ubaya wowote._Methali 3:27-30

WATEMBELEAJI