Mtu mmoja wa Kongwa - Dodoma....alipata nafasi ya kwenda Ulaya kusoma, alipomaliza kusoma akapata kazi huko huko Ulaya. Alikaa miaka 20 bila kurudi nyumbani.....siku moja akarudi nyumbani; mahawala zake watatu aliyowaacha zamani akawakuta....mmoja mchaga, mwingine mmasai na mgogo wa Dodoma. Wakampeleka Baa fulani maarufu Dar es salaam, wakachagua meza ya kukaa.....muudumu akaja na kuwauliza wanataka nini; mchaga akaagiza KILIMANJARO LAGER, mmasai akaagiza SERENGETI LAGER, na mgogo wa Dodoma akaagiza DODOMA WINE.
Jamaa huyo wa Kongwa, akafikiria kimoyomoyo; siku hizi Tanzania kila sehemu kuna pombe yake. Kwa mbwembwe zote na kwa sauti kubwa akasema; lete KONGWA LAGER baridi!!!!!!!
No comments:
Post a Comment