Tuesday, January 22, 2013

FR.JOAKIM NDELIANARUA MINJA......NITAKUKUMBUKA DAIMA! PUMZIKA KWA AMANI.

Leo saa 10 jioni, nilipofika tu! uwanja wa ndege Dar es salaam....nikitokea huko nchini Italy, nikapata simu kutoka kwa rafiki yangu mmoja na kunipa taarifa ya msiba wa Fr.Joakim Ndelianarua Minja, sisi tulimzoea kumwita Fr.Ndeli. Pichani hapo na kibuyu enzi za uhai wake.
Kwakweli nimesikitishwa sana na msiba huu mzito, maana ni msiba wa ghafla sana...nilikuwa sina taarifa kuwa anaumwa wala nini, wamesema kafariki ghafla tu! huko Parokiani Mbezi Beach - Dar es salaam, ambako alikuwa akifanyia utume wake.  Fr. Ndeli, nilikuwa na mfahamu sana kwa ukaribu sana. Kutokana na mimi kuwa na urafiki sana na Mafather wote wa Shirika la Damu azizi ya Yesu (Precious Blood Fathers). Maana alikuwa akija tu Italy, mara nyingi tunaonana.
Alishawahi kuwa Mkubwa wa Shirika hili kwa ukanda wa Tanzania, Fr.Ndeli alikuwa mcheshi sana.
Kwasasa tunasubiri ratiba nzima ya mazishi yake, kwakweli ni majonzi makubwa sana!

Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu Padri Ndeli....mahali pema peponi, amina!
Sisi tulikupenda.....lakini Mwenyezi Mungu kakupenda zaidi Fr.Ndeli.

No comments:

WATEMBELEAJI