Friday, March 29, 2013

LEO NI IJUMAA KUU.....ADHIMISHO LA MATESO YA BWANA WETU YESU KRISTU.

Ee Bwana, kumbuka rehema zako, uwatakase watumishi wako kwa ulinzi wako wa siku zote. Kwa maana Mwanao Kristu aliwawekea fumbo la Paska kwa damu yake. Anayeishi na kutawala milele na milele....Amina!

Ee Mungu, kwa mateso ya Kristu Mwanao Bwana wetu umetuondolea mauti tuliyorithi sisi binadamu wote kwa dhambi ya kale. Utujalie sisi tuliozaliwa na hali ya kibinadamu kwa maumbile, vivyo hivyo tuzaliwe na hali ya kimungu kwa kutakaswa na neema yake.

- Ijumaa kuu njema kwenu nyote!

No comments:

WATEMBELEAJI