Sunday, June 23, 2013

NIMEMPIGA CHENGA YA MWILI SHETANI.......JUMAPILI NJEMA.

Nimempiga shetani chenga ya mwili, ili kuisalimisha Roho yangu.....nimempokea Yesu moyoni mwangu nipate uzima wa milele ili niishi milele.
Tazama nimebatizwa kwa nafsi tatu; Baba, Mwana naye Roho Mtakatifu.....nimempokea Kristo moyoni mwangu, kwa mwili na damu yake nimeshibishwa.
Nimepokea Roho Mtakatifu, amenijaza mapaji saba......nimeikiri imani yangu, nimemkana shetani na mambo yake yote.
Nikikumbuka kiapo cha ubatizo wangu najionea fahari ukristo wangu, nikikumbuka ungamo la dhambi zangu, ninaukiri upendo wa Yesu Kristo.
Nimeshamweka kando shetani mwovu, aliye mpotoshaji wa mambo mema.....alishaniweka kwenye himaya yake, alinidanganya sana na vishawishi.

No comments:

WATEMBELEAJI