Wednesday, August 7, 2013

HAYA NDIYO MALEZI MAZURI SANA, YA KUJIFUNZA KAZI ZOTE....PIA NI MSAADA SANA KWA MAISHA YA HAPO BAADAE HUWEZI JUA.



- Hongera sana Dada yangu Yasinta, kwa malezi mazuri kwa wajomba......malezi ya kuwafundisha kazi watoto pia ni muhimu sana tena sana katika haya maisha, maana hapo baadae wanaweza kujitegemea bila shida yoyote. Lakini kama hawajui kazi inabidi waanze kujifunza na kuhangaika huku na kule. Ni muhimu sana kuwafundisha kazi watoto, ili hapo baadae iwe rahisi sana kwao kujitegemea. Kuna watoto wengine hawajui hata kuinua kikombe cha maji ya kunywa.....eti wazazi au walezi wanasema ndio upendo, upendo gani huo?
Hizi picha nimezipenda sana, ndio maana nikaamua niziweke na hapa.
- Asante sana Dada Yasinta.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka baraka ahsante nawe . Kumbe nawe ni mpekuzi.-:)

WATEMBELEAJI