Tuesday, August 20, 2013

ITAKUWA KAMA NDOTO SIKU YA KUFA KWANGU!

Itakuwa kama ndoto pale moyo wangu utakapozima kama mshumaa uliopulizwa na upepo. Utatamani niamke angalau usikie sauti yangu, lakini utakuwa tayari umeshachelewa........kilio, huzuni, simanzi na majonzi zitakuwa zimetanda katika kuta za moyo wako. Machozi yatakutoka kila utakapokumbuka ucheshi wangu na moyo utakuwa mpweke kila utakapoiona namba yangu kwenye simu yako....utatamani uifute ila roho itakuuma sana kwa kuwa umenizoea sana.

- Hivyo jaribu kufurahia uwepo wangu kabla sijatoeka duniani.....kwani chura anajua umuhimu wa maji baada ya maji kukauka. Tupendane jamani, maisha yenyewe ya hapa duniani ni mafupi sana!

No comments:

WATEMBELEAJI