Tafakari sana juu ya neno maisha, elewa sio kila mtu anae cheka na wewe na kufurahi na wewe ukadhani ndio rafiki wa kweli. Utu wao umo katika macho.........lakini nafsi zao zimebeba; Husuda, Uadui, Uchawi, Uchoyo na roho mbaya.
Furaha zao kukuona unaharibikiwa, na hasira zao kukuona unafanikiwa......wangapi uliwaamini, ukawapenda, ukawasaidia, ukawaona ndugu, ukawapa siri zako? Leo ndio maadui zako?
- Kweli maisha ni watu, lakini kuwa mwangalifu sana nao........kuwa mwangalifu nao sana tu!
No comments:
Post a Comment