Friday, December 4, 2015

HII NI DHANA KONGWE YA KIMTAZAMO ILIYOJENGEKA KIFALSAFA.

Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa....ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana.
Huvyo; inahusu uwezo kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti, ndio kuna kuona kikiwa na kuona kama; kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti. Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ''Paradigm Shift'' ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captan Thomas Sankara, kiongozi mwana mapinduzi aliyeuawa Burkina Faso, katika wakati wake.....alizungumzia umhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale. Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani; mwanamapinduzi huyu alikuja kuuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.
Sankara alipata kukaririwa akisema; ''Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni....basi tunastahili ushindi, kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshindikizwa na taratibu zilizo zoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mstakabali...ni wendawazimu wa jana uliotuwezesha kufanya tuyafanyayo leo hii. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao'' (Hayati Captan Thomas Sankara). 

Yamkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's Paradigm Shift; Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi.....kuna wanao mshangaa Rais John Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, yawezekana Magufuli anaonyesha kwa Mawaziri wake wajao, nchi inaweza kwenda bila uwepo wa Mawaziri Miungu watu;......wakifanya mchezo wanatimuliwa tuu, kwani nchi yaweza kwenda hata bila wao. Na hii ya Magufuli Paradigm Shift inaweza kuibadili nchi kwa haraka, maana kila mmoja atalazimika kubadilika.

No comments:

WATEMBELEAJI