Tuesday, December 22, 2015

KIPA HUYU AMECHUKIZWA SANA NA MAMBO YALIYOPO NDANI YA MCHEZO WA MPIRA, KAKERWA SANA NA MAMBO MENGI NA KUAMUA KUWEKA HADHARANI MAMBO NA KUACHA KABISA MCHEZO HUU WA MPIRA.

Kipa maarufu wa hapa Nchini Italia, Kipa wa timu ya Fiorentina, ndugu Frey......ameamua kuacha kabisa kucheza mpira kutokana na mambo yaliyopo kwenye mpira mabaya na yanakera sana, yeye kasema amevumilia mwisho ameshindwa kabisa hivyo ameamua kuachana nayo kabisa na mambo haya ya mpira. Na kaamua kusema hadharani kabisa bila kuficha chochote.
Namnukuu anavyosema hapa;

- Naacha kabisa kucheza mpira, nimechoka kabisa. Miaka mitatu au minne iliyopita nimegundua kuwa dunia hii ya mpira inanihusu kidogo sana. Vijana wa leo wenye miaka 11 na kuendelea wanafikiri kuwa kama Messi, au Cristiano Ronaldo. Nataka niwe na gari la kifahari, viatu ambavyo vina jina lake juu, badala ya kufikiria kucheza mpira. Mimi sijui nitasemaje nikirudi miaka nyuma ambapo unawaza kuchukua mpira na kwenda kucheza na marafiki tu. Ndo yalikuwa mawazo yangu pekee kichani, kuwa mchezaji  mpira yalikuwa maisha yangu, lakini sasa siwezi kwenda uwanjani, kuchukua mshahara tu.

No comments:

WATEMBELEAJI