Friday, December 11, 2015

MABABA HAOOOO.......HAPA KAZI TU SASA! TUMEPATA MA BABA WA UKWELI TANZANIA.

Ndugu yangu Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya awamu ya tano. Vinaonekana vita unavyopigana kuwakomboa wanyonge walio wengi wa nchi hii. Kazi unayoifanya hadi sasa inadhihirisha wazi kabisa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli, hajakosea katika kulichagua ''Tingatinga'' la ukweli la kumsaidia kwenye kazi yake hii ya uraisi.
Hapo bandarini yaonekana kuna mashimo mengi ya panya wanaotafuna mapato ya nchi yetu hii. Na wengine ni mapanya Buku mithili ya ukubwa wa sungura. Eti wanasema '' Bandari kavu'' kumbe zimejaa mashimo ya panya. Iko wapi NASACO ya Watanzania? Miaka 54 ya Uhuru kwanini tushindwe wenyewe kuendesha Bandari ya majini na nchi kavu badala ya kuwaachia panya wafanye kazi hiyo?
Ewe Majaliwa mwema, vita ya panya wa Bandarini kamwe isiwe na matokeo ya kutoka sare. Pambana na panya wezi na wenye kuficha mali zilizoibiwa na panya wezi wenzao. Ukitoka hapo Bandarini na ushindi wa jumla, basi tutasonga mbele na ukiwa na nguvu zaidi, na umma ulio nyuma yako katika kumsaidia Rais kwenye vita ya pili ya ukombozi wa kiuchumi kwa nchi yetu tuliyozaliwa na kuipenda sana Tanzania.

No comments:

WATEMBELEAJI