Wednesday, December 9, 2015

MAJANGA YA MOTO KATIKA MISITU YA MAFINGA, IRINGA - TANZANIA.


Mwezi uliopita nilikuwa huko Makalala, Mafinga - Iringa, ambapo moto mkubwa sana ulizuka kwenye msitu wa Jeshi na kusambaa kuja hadi karibu na kituo cha watoto yatima cha Makalala ambapo nilikuwa nimefikia hapo. Ilikuwa ni balaa kuuzima......tulikuwa tukiuzima kwa kutumia matawi ya miti wengine kwa maji, tulipambana na moto huo mpaka saa nane na nusu usiku kuanzia saa mbili usiku, tukafauru kuuzima. 
Lakini ilikuwa patashika ya kutosha sana......hii ni baadhi tu ya ushenzi wa watu wenye roho mbaya huwasha kwa makusudi kabisa misitu hii ya mbao, labda wanaomba kuuziwa miti hii ili kuvuna mbao halafu wewe unakataa...kusema; bado siuzi kutokana na malengo uliyojiwekea binafsi....hapo ndipo wanachukia na kuchukua hatua mbaya kama hizi za kuwasha moto, ili miti yote iteketee ili mkose wotee!!!!
- Sasa hii ni akili au matope?

No comments:

WATEMBELEAJI