Thursday, December 3, 2015

MUHINDI KATIKA KUTAFUTA HELA.......JIJINI ROMA, NCHINI ITALY.








Muhindi huyu yupo katika kusaka hela katika mitaa ya Roma - Italy, niliipenda sana hii....maana mpaka ugundue kama kaweka chuma ambalo linapita mkononi na kuzunguka mgongoni mpaka kwenda kwenye makalio ambako kuna kitako alichokalia, utakuwa tayari umeshafurahi sana. Utafikiri kweli kakaa anaelea elea juu, kumbe ni mbinu na ubunifuu tuuu......hapa kupiga picha nae lazima uangushe hela chini kwenye kibakuri kidogo kilichopo chini mbele yake, na kuna mtu pembeni anaelinda na kuruhusu kupiga nae picha, kama huweki hela anakutimua hakuna kupiga picha. 
Maisha ni kutafuta bwana, si kutafutana! Anajipatia tu ridhiki yake mdogo mdogo.....niliipenda sana hii nikajikuta naagusha euro zangu mbili kwenye kibakuri, hapa ni moja ya mitaa ya kati ya Jiji la Roma, majuzi kati nikiwa huko kutembea.

No comments:

WATEMBELEAJI