Sunday, January 31, 2016

KUKATA TAMAAA NI MWIKO KABISA KWA SISI BINADAMU!

HATA YESU MWENYEWE ALISEMA;

Mwenyezi ameniumba, akanileta  kati yenu niwakumbushe watu wake dhamani yenu duniani. Achani kufa moyo, acheni kukata tamaa yeye aliyewaumba anaijua kazi yake.

Aliijua siri yenu hata kabla hamjaumbwa, thamani ya maisha yenu yote ipo mikononi mwake, magonjwa yanayo watesa na maumivu yasiyo koma......ni madogo kuliko yale aliyoyaponya kwa sekunde.

Hali mbaya ya kiuchumi muda mmoja madeni mengi......ni njia ya kunyenyekea na kumpa Mungu utukufu. 
Misiba inayowaliza mnapofiwa na ndugu zenu......ni njia ya wapendwa wenu kwenda mbinguni wakafurahi.

Maumivu ya kuonewa, kudhurumiwa, kusingiziwa......ni nafasi ya kusamehe na kujitwika Utakatifu. Matatizo ya ndoa zenu na migogoro ya familia......ni bahati mmejaliwa ya kujifunza uvumilivu.

Bebeni misalaba yenu na nyamazeni msinung'unike......huu ndio wokovu wenu shikirieni msiachie.

No comments:

WATEMBELEAJI