Saturday, July 9, 2016
YAANI MADEREVA WA MABASI WA HAPA KWETU HAWAJALIKABISA, WANAYACHAKAZA KILA KUKICHA LAKINI HAWAJIFUNZI KABISAAA!!!!!!
Siku moja nimepanda basi, tukakuta ajali mbaya sana ya kusikitisha....yakiwa yamehusishwa magari matatu, mabasi mawili na lori moja, kwakweli ajali hiyo ilikuwa inatisha sana. Lakini baada ya kuipita ajali hiyo mbele kudogo dereva wetu akaanza mbwembwe za kuendesha vibaya, kuovateki vibaya kwenye milima ambapo mbele haoni vizuri kama gari inatokea. Kwakweli nilisikitika sana na kujikuta naenda kumwambia dereva kuwa umeona ajali mbaya dakika chache tu zilizopita, na sasa wewe unafanya nini hii? Alinijibu ajali ni ajali tu! Kwakweli nilisikitika sana na kuona jinsi gani Watanzania ambapo hatujali uhai wetu na maisha yetu kwa ujumla. Mungu kakupatia uhai kwa ghalana kubwa sana, kwanini usijali uhai huu? Kwa kuulinda kwa ghalama kubwa ya juu?.... Kwakweli madereva wa mabasi ya Tanzania walio wengi sana hawajali uhai wa maisha ya watu....madereva tunaomba sana mbadilike jamani, mnabeba watu sio magunia jamani....mnamaliza sana ndugu zetu wasio na hatia yoyote...chonde chonde madereva wa mabasi muwe wastarabu barabarani na kujali maisha ya watu wenye ndoto zao nyingi za maisha, kuliko kukatisha hizi ndoto zao za maisha, salimsheni haya maisha jamani tunaomba sana sanaaaa.....!!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment