Maombezi yako Mama Maria kwa mwanao mpendwa, yatupatia faraja siku zote.
Sala zako Mama Maria kwa mwanao mpendwa, zatupatia nguvu na faraja mioyoni mwetu.
Fadhila na matendo yako Mama Maria yatupatia tumaini maishani mwetu.
Uzidi kutuombea Mama mwema, tupate neema ya kuepuka maovu, utuweke mikononi mwako Mama, tufuate njia ya mbinguni kwa amani.
Asante sana Mama Maria mwenye huruma kwa kutusimamia sisi wana wako, hatuta kuacha kamwe Mama Maria, tutakukimbilia wewe siku zote daima!
No comments:
Post a Comment