Saturday, March 11, 2017
KWENDA KWA BIBI MZAA MAMA YANGU....LAZIMA UKUTANE NA HUU MTO. KUVUSHWA HAPA KWA MTU MMOJA NI SHILINGI 1000.
Hapa ilikuwa jana, juzi usiku nilienda kwenye kumaliza msiba wa mama yangu mkubwa, nikakuta mto umejaa balaa, huwezi vuka na gari...na ilikuwa lazima nifike kijijini huko, ndipo nikavushwa kwa shilingi elfu moja, wapo vijana wa kazi hiyo, ni wazoefu balaa. Na ukiyadharau maji lazima yakupeleke. Na mto huo umeua watu wengi sana kwa kudharau, maana unapitisha maji kwa kasi sana. Jana wakati nikirudi zangu nikakuta yamepungua sana, huwa linapitisha kwa haraka sana maji....jana ndipo nikavuka mwenyewe tu bila kuvushwa, maana yalishapungua sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment