
Gari la kubebea wagonjwa ''Ambulance'' likiwa karibu na tukio tayari kutoa msaada kwa majeruhi.
Ndege ya abiria iliyokuwa imebeba watu 90 imeanguka katika bahari ya Mediterranean. Ndege hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa Beirut nchini Lebanon.Ripoti zinasema ndege aina ya Boeing 737 inamilikiwa na shirika la ndege la Ethiopia. Maafisa mjini Beirut wanasema ndege hiyo ilipoteza mwelekeo takribani dakika 30 baada ya kupaa angani. Watu wanaoishi karibu na bahari ya Mediterranean wameripoti kushuhudia ndege hiyo ikianguka baharini huku ikiwaka moto. Inasemekanakuwa abiria 50 ni raia wa Lebanon huku wengine raia wa Ethiopia.
No comments:
Post a Comment