Monday, March 29, 2010

POLISI WANAWAKE WAENDA DARFUR - SUDAN.

Kundi la kwanza la Polisi wanawake, limeondoka nchini kuelekea nchini Sudan kwaajili ya kuongeza nguvu katika maswala ya kulinda amani katika eneo la Darfur.

Akizungumuza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa askari hao, kwa niaba ya mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, mkuu wa utawala kamishina Mwandamizi SACP Zuhura Munisi, amewaasa askari hao kwenda kuzingatia maadili ya kiutendaji kazi yao, ili kuleta heshima ya Taifa letu mbele ya sura ya Umoja wa Mataifa.

Kamanda Munisi amesema kuteuliwa kwa askari wanawake kwenda kulinda amani nchini Sudan kunatokana na ukweli kwamba wengi wa wahanga walioko katika maeneo yanayokubwa na migogoro nchini humo ni wanawake na watoto, hivyo itasaidia sana kwa uwepo wa askari wa kike.
Kamanda Munisi amewakabidhi Bendera ya Taifa askari hao, kwa mkuu wa msafara huo Mrakibu wa Polisi Hawa Luzy.

-Kila lakheri nyingi sana na mafanikio mengi ya kuleta amani nchini Sudan, kwa askari wetu wa kike wa Taifa letu, safari njema na kazi njema sana!

SOURCE; MHINA WA POLISI.

No comments:

WATEMBELEAJI