Friday, April 16, 2010

WENYE MAKOSA MADOGO MADONGO KUPEWA KIFUNGO CHA NJE.

Katika hali ya kuonekana kuna msongamano wa wafungwa gerezani, kwa hali hii Serikali imeamua wafungwa wenye makosa madogo madogo kutumikia kifungo cha nje ili kuepuka msongamano huo.
Wafungwa hao watatumikia kifungo cha nje, adhabu zao kwa kufanya kazi mbalimbali za Jamii huku wakiishi uraiani. Mpango huo ulio chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, imeendelea kuwapatia mafunzo Maafisa wake kwa huduma za Jamii ili waweze kusimamia sheria zinazotoa fulsa kwa wafungwa hao kutumikia adhabu zao uraiani.

Mkurugenzi wa huduma ya Jamii wa Wizara hiyo, Onel Malisa, alisema mbali na kupunguza msongamano wa wafungwa hao, pia adhabu hiyo itasaidia kupunguza gharama kubwa za kuendeshea Magereza.
Wafungwa watakao tuhumiwa adhabu hiyo itawahusisha waliohusika na makosa kama ya wizi wa kukwapua, wanaoiba kuku, wenye kutoa lugha ya matusi na nyingine nyingi ndogo ndogo zinazoendana na hizo. Alisema wafungwa hao watapangiwa kazi za kutunza mazingira katika vyanzo vya maji, ujenzi wa shule, kufagia barabara, kuzibua mitaro ya maji machafu, kupangiwa kufangia ofisi mbalimbali, n.k. Kwa kusimamiwa na maafisa wa huduma kwa Jamii nchini.

No comments:

WATEMBELEAJI