Tuesday, May 25, 2010

BONGO-TZ: MAMBO YOTE YANAWEZEKANA TU BILA SHIDA.

Hapa ikitokea ajali ni mpango ya Mungu tu, au ni kazi ya Mungu tu! Wapi na wapi ni kazi ya Mungu? Ni kazi ya mwanadamu tu, anafahamu kuwa ni hatari lakini ndo hivyo tena, pia ni maisha yetu ya kiumaskini tunalazimika kusafiri na kifo mkononi. Ila tusiseme ni kazi ya Mwenyezi hii hata kidogo. Na vile vile Mungu ana kazi sana kutulinda na hatari kama hizi, ashukuliwe sana Mwenyezi wetu.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli hapo wa kumlaumu ni nani lakini pamoja na umaskini wetu kuchanganya mizigo na watu ni HATARI sana na hairuhusiwi kabisa. Watu wanachukulia kila kitu rahisi rahisi tu kumbe wanajipeleka kaburini wenyewe. Mungu uwe nasi, Upendo daima!!

WATEMBELEAJI