Friday, May 28, 2010

HII INASABABISHWA NA UNYAFUZI WA AKILI AU?

WASHINDWA KULIMIA MATREKTA, KISA? HAYAJAZINDULIWA NA RAIS!

Wakulima 417 katika bonde la mpunga la Mtwango - Zanzibar, wamekwama kutumia Matrekta mapya katika msimu wa kilimo unaomalizika mwezi huu, kwasababu hayajazinduliwa na Rais wa Zanzibar, Amani Karume.

Uchambuzi wa gazeti la Nipashe umegundua kwamba Matrekta hayo yaliwasili Zanzibar tangu Julai mwaka jana kutoka nchini Italia.
Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya wakulima wakisema wamekwama kutumia Matrekta hayo baada ya watendaji wa Wizara ya kilimo kudai hayawezekani kutumika kabla ya kuzinduliwa na Rais.

YATOKANAYO;

Iko shida. Naona iko shida. Nasema ni shida kubwa. Shida kubwa sana. Sasa tunaweza kujaribu kuelewa ni kwanini viongozi wanashindwa kuongoza Wananchi. Hawafanyi kinachotarajiwa, tunasubiri bado kupokea amri na kusukumwa kama watumwa. Iko shida. Naam iko shida. Shida kubwa sana. Sasa tunaweza kujaribu kuelewa ni kwanini aliyasema 'uongozi ni mzigo' aliyasema hayo; aliyesema kwamba ''hakuna umaskini mbaya kabisa kuliko umaskini wa akili'' hakukosea kabisa. (Aliyeyasema hayo ni marehemu Mwalimu Nyerere).
Elimu na maarifa ni nguzo muhimu sana maishani mwetu.

-Wavuti.

No comments:

WATEMBELEAJI