Saturday, May 15, 2010

MAISHA YA BIN'ADAM!

Katika maisha yake yote Bin'adam hana budi kufahamu ana jukumu gani akiwa kama kiumbe katika hii Dunia. Suala hili linakuja pale Binadamu huyu anapojitambua hakuwezekana mpaka Binadamu huyu aweze kujibu maswali haya;

Mimi ni nani?
Ninatoka wapi?
Niko wapi na kwanini?
Ninaelekea wapi?
Mwisho wangu utakuwa nini?

Haya ndio tunaita maswali ya msingi sana. Binadamu anapoweza kujibu maswali haya na akazingatia majibu yake tunasema amejitambua, ibaki utekelezaji tu!
Katika utendaji wa kitu chochote, kujitambua ndio jambo la msingi la kwanza kabisa. Kwa mfano; Meneja hawezi kuwa ni Meneja mzuri kama hajitambui, kwa maana kwamba haelewi ili kuwa Meneja anatakiwa awe vipi na afanye mambo gani yanayomuwajibikia. Hivyo hivyo Binadamu huyu hawezi kuwa muumini safi kama haelewi Binadamu anatakiwa aweje na aishi vipi.

-Baraka wa Chibiriti.

No comments:

WATEMBELEAJI