Monday, May 31, 2010

MARA GHAFLA UWANJA MZIMA KIMYA KUSIKILIZA MATOKEO.


Mara ukimya ukatawala uwanjani Piacenza, wengine wakisikiliza redio za masikioni, baada ya kuisha mechi yetu na Cesena kushinda kwa bao moja kwa sifuri, lakini isingelitosha kwa ushindi huo wa Cesena. Ilibidi kusubiri mechi mhimu ya huko Padova - Brescia iishe, na kulikuwa bado na dakika 5 ili mechi hiyo iishe. Mashabiki tulianza kupata wasiwasi mkubwa tukisubiri matokeo ya huko Padova. Mara baada ya dakika 5 kuisha sherehe ya Cesena ikaanza kwa kishindo, nilihisi kama vile jukwaa lingeanguka kwa furaha ya mashabiki wa Cesena, baada ya kusikia Padova imeshinda bao 2-1 dhidi ya Brescia, ambayo ilikosa pointi moja tu...watuzidi kwa kupanda daraja, lakini walishindwe kupata hata hiyo pointi kwa kutandikwa 2-1. Hapo ndipo sherehe kubwa sana ilipo anza kwa sisi mashabiki wa Cesena.




Jamaa zangu Cappo na Hulio, wakiandaa gari kwa urembo wa mbwembwe kali za kupanda daraja, kutoka daraja la pili (Serie B) kwenda daraja la kwanza (Serie A). Hapa tunajiandaa kurudi Cesena kwenye sherehe ya kweli hapo mjini Cesena.



Dereva wetu Cappo, alishindwa kuendesha kabisa, kwa furaha alizo kuwa nazo...ghafla alianza kulia..(Mimi nimecheka sana) Lakini hakuwa yeye peke yake aliye lia, wengi niliona wamelia sana. Tulijaribu kumnyamazisha Cappo, hatukufanikiwa na tulichelewa kuondoka karibu saa nzima ilipita. Ikabidi kura ziniangukie mimi kuendesha kurudi Cesena. Tulikuwa watano ndani ya gari barabara yote ni fujo tupu, fujo za furaha. Lakini Mungu alitulinda tukafika salama kabisa bila shida yoyote.





Hapa sherehe ndio inaishia ishia hivyo...!!!




Tuliwasili Cesena saa tatu na nusu usiku, barabara zilikuwa zimejaa magari, matrekta, pikipiki, malori n.k. Kusheherekea ushindi huu. Tulipata bahati sana kubaki nyuma ya Gari la Polisi ambalo lilikuwa kwenye msafara wa basi la wachezaji wa Cesena....tuliwafuata mpaka tukafika nao uwanjani, ila ilikuwa si kazi rahisi..lakini tulifika nao.
-Mwezi wa nane mwishoni ligi ya Italia itaanza, na tunawasubiri kwa hamu wale wa timu kubwa; Ac.Milan, Inter Milan, Juventus, Roma, n.k. Itakuwa ni furaha sana, kuziona hizi timu kubwa hapa Cesena.







No comments:

WATEMBELEAJI