Saturday, May 15, 2010

NAPENDA KUWAAGENI WADAU ZANGU WAPENDWA SANA!

Napenda kuchukua nafasi hii, kuwaageni ninyi nyote wadau zangu wapendwa sana katika kijiwe hiki cha; KAZI YAKO NI JINA LAKO. Nitasafiri kidogo kikazi na nitakuwa bize sana kwa wiki lote hili lijalo, pia ninakoenda mara nyingi mtandao huwa unasumbua sana kupatikanika maana ni sehemu za milimani. Kwahiyo nimechukua uamzi wa kutokwenda na computer maana ni usumbufu tu, kwasababu hiyo ya usumbufu wa mtandao, na pia mimi kuwa na ubize mkubwa. Basi tutaonana wiki inayo fuata.

Nategemea kuondoka hapa Cesena baada ya saa moja ijayo, ndipo nitaanza safari yangu hii yenye mvua nyingi na baridi kwa wingi. Baada ya wiki moja nitarudi na tutaendelea na libeneke kama kawaida, naomba sana msinikimbie, mimi nitakuwa nawakumbukeni sana kwa sala na mawazo ya kuwawaza daima ninyi nyote wadau zangu wapendwa.

Natanguliza samahani zangu sana tena sana...kwa jambo hili, maana wengi watanimiss hata mimi hivyo hivyo kwenu ninyi nyote.

NAWATAKIENI MAISHA MEMA SANA, KILA LAKHERI KWA WIKI IJAYO.
NA TUTONANA TENA MUNGU AKIPENDA... KWA HABARI NA MAMBO MBALIMBALI KAMA KAWAIDA, WIKI INAYOFUATA. NIPO PAMOJA NANYI DAIMA!

NI MIMI YULE YULE WA KILA SIKU;
BARAKA WA CHIBIRITI.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nami napenda kuchukua nafasi hii na kukutakia SAFARI NJEMA SANA NA KILA UTAKALOFANYA liwe safi MWENYEZI MUNGU AWE NAWE NMI NIPO NAWE KWA SALA .UPENDO DAIMA

ray njau said...

Machozi ya furaha na kigugumizi cha shangwe kutoka ndani ya moyo wangu.Nikutakie baraka tele,afya njema na kila lililo jema liambatane na safari yako.Wasalimie wadau wote huko na usisahau kuwaambia kuwa nawakaribisha kwenye huduma za forodha hapa Dar es salaam.

WATEMBELEAJI