Monday, May 10, 2010

NENO ''BOMB'' LAMPONZA MRUNDI NDANI YA BASI .

Neno ''BOMB'' lamponza Mrundi aliyekuwa akizungumza Kiswahili ndani ya basi huko Marekani;

Ilitokea huko Nchini Marekani kwenye basi la abiria la masafa marefu, al maarufu (Greyhound) pale mtu mmoja raia wa Burundi ndani ya basi hilo alipokuwa akizungumza na mwenzie kwenye simu, na bahati mbaya aliyekuwa kakaa nae jirani kwenye basi hilo akasikia kama vile ''Bomb'' linatamkwa mara kwa mara, kumbe jamaa akisema kwa kiswahili ''Bobu'' hivyo jirani huyo akapiga simu katika kituo cha Polisi cha kuomba msaada wa dharura ''911'' kusema kuwa amesikia habari ya kuwepo kwa Bomu ndani ya basi hilo.

Ilibidi safari isitishwe na watu wote walitolewa kwenye basi hilo, lakini aliyekuwa akizungumza na simu Mrundi huyo, aligoma kutoka ndani ya basi hilo na alibaki humo kwa saa nane, wachilia mbali juhudi za askari kumsihi atoke, hadi pale Polisi walipofanikiwa kumpata ndugu yake aliyekuwa akiongeanae kwenye simu kwa kiswahili. Ndugu yake huyo ndipo alipo thibitisha kuwa usalama wake haupo hatarini kabisa, kwani ni mtu mwema kabisa na wala hana Bomu. Polisi walisema huenda mtu huyo aliogopa sana kutokana na historia ya alikotoka kuwa ya vita na vitisho vikubwa vya askari dhidi ya raia.

-Kazi kweli kweli!!!

-Kutoka kwa WAVUTI.COM

No comments:

WATEMBELEAJI