Monday, May 31, 2010

SAFARI YETU YA KWENDA PIACENZA KUSHANGILIA ILIANZIA HAPA!

Baffo na Hulia....wakipanga panga mizingo tayari kwa safari yetu ya kwenda Piacenza kuishangilia Timu yetu Cesena ili ipande daraja, ilikuwa jana Jumapili.
Cappo na Hulia, tulipo simama kujaza Gesi kwenye Gari letu la ushabiki, baada ya kusafiri km.180, jana sehemu za kujazia mafuta au Gesi palikuwa hapatoshi, mashabiki wa Cesena walitawala barabara nzima...sijapata kuona, kila tulipo simama kwenye kujaza Gesi hatukuweza kufanikiwa kutokana na foleni, baada ya stesheni 4 ya 5 tukafanikisha.

Radichio, akaipenda sana gari hii....naomba nipige picha, naomba nipige picha, mimi namkaukia tu...mpaka nikamkubalia. Gari tuliikuta kwenye Parking High Way Bologna - Piacenza.



Mashabiki mashabiki mashabikiiii....kwa wingi wote tukielekea Piacenza kuipa nguvu Cesena. High Way - ya Cesena - Piacenza km 286, karibu yote ilijaa magari na mabasi ya mashabiki wa Cesena, bendera na jezi za Cesena zilitawala sana kila gari. Kwa ripoti ya magazeti tulikuwa 8400.



Nikashangaa naitwa kwa nguvu zote....Baraka Barakaaaa....kugeuka jamaa tunafahamiana sana, kushoto Francesco na mdogo wake. Yeye aliniambia kabla asingeweza kufika, maana alikuwa kazini...lakini akasema ni heri hata afukuzwe kazi, kuliko asishuhudia Cesena Ikipanda daraja, mimi nikamwuliza unauhakika gani kama itapanda daraja? Nasikia kutoka moyoni na mwilini ndio maana sijaenda hata kazini...Kazi kweli kweli....!!!!



Tukafika Piacenza baada ya kusafiri km 286 kutoka Cesena. Baada ya kufika tu kitu cha kwanza chakula kabla ya kuingia uwanjani. tulikuwa full kila kitu tunacho mpaka jiko dogo la kupikia, hapa kwenye Parking hii ya mashabiki wageni, jana ilikuwa kama pick nick yaani ilipendeza sana.





No comments:

WATEMBELEAJI