Tuesday, June 1, 2010

HII NI HARUSI YA KISIMPO TUU...LAKINI POA KABISA.

Harusi yako inatakiwa iendane nauwezo wako...si kujionyesha ufahari tu, wakati huna uwezo. Fanya sherehe, furahi, shangilia hivyo hivyo kadiri ya uwezo uliyo nao sio baada ya sherehe unajikuta una madeni na hujui utayalipaje...kweli utaanza maisha vizuri kwa kuanza na madeni? Asikudanganye mtu...sherehe ni sherehe tu! cha muhimu ni kufurahi na wenza wako, na watu wote (waalikwa). Mimi binafsi hii picha nimeipenda, maana inamafunzo ndani yake. Nchi yetu ni maskini lakini unashangaa kuona hausi zinavyo kuwa za kifahari, wakati wenzetu matajili lakini hatuoni ufahari huo wakati wa harusi zao. Kazi kweli kweli....!!!!!

2 comments:

ray njau said...

Asante kwa taswira nzuri ya kijamii Baraka mwwenye baraka.Ni vema uwaulize wakuambie ni kwao ni chenye thamani na harusi au sherehe ya harusi?Nauliza hivyo kwa kuwa katika jamii yetu michango ya harusi ndiyo imepewa nafasi kubwa maishani na hakuna michango kabisa kwenye maeneo ya kijamii kama elimu,afya na miundo mbinu ya mawasiliano kwa ujumla.Mambo hayo yameachwa mikononi mwa serikali kuu na sserikali za mitaa.

Baraka Chibiriti said...

Ni kweli kabisa Mkuu Njau, hata michango ya wagonjwa wetu mahospitalini ili watibiwe vizuri na kupona ili tuwe nao tena hapa duniani...hatukumbuki kabisa kuhusu jambo hili mhimu sana la kuwachangia watu wakosapo pesa ili watibiwe. Ila mtu akifariki utaona watu wanajitokeza na kutoa michango, sasa inasaidia nini..wakati mgonjwa hakupata huduma, na wakati mwingine anakosa hela kidogo tu, ili aweze kupata huduma nzuri. Kila kukicha tunaombwa michango ya harusi tu, je wagonjwa wetu vipi?

WATEMBELEAJI