Thursday, June 3, 2010

LINI TUTAJIFUNZA KUKABILIANA NA UCHAFU KAMA TISHIO??

Hivi kweli tutajifunza lini kutunza mazingira yetu, ambayo tunaishi sisi wenyewe. Mbona wenzetu hawawi hivi, ina maana wao sio binadamu ??? Au???? Kwanini na sisi tusiweze kutunza mazingira yetu?


Wakazi wa Chamwino kwa Mgulasi karibu na Klabu cha pombe za kienyeji, katika Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro wanakabiliwa sana na athari ya kupatwa na magonjwa ya mlipuko hasa Kipindupindu kutokana na lundo la uchafu wa aina mbalimbali uliozagaa kwa kipindi kirefu, kuoza na kutoa harufu mbaya sana, kama ulivyokutwa katika eneo hili.

Lini tutajifunza kuwa wasafi katika mazingira tunayoishi????

No comments:

WATEMBELEAJI