Wednesday, June 9, 2010

MABASI YA WANAFUNZI YAZINDULIWA DAR ES SALAAM.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makongo - Dar es salaam, wakipanda kwenye moja ya mabasi mapya ya wanafunzi mara baada ya Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda, kuzindua huduma hii ya usafiri ya mabasi hayo matano ya wanafunzi wa Dar es salaam yaliyotolewa na Benki ya CRDB Jijini Dar es salaam.
TUKIAMUA INAWEZEKANA KUIONDOA ADHA HII KWA WANAFUNZI;
Asante sana Benki ya CRDB kwa kuzindua mradi wa mabasi ya wanafunzi, naamini adha kama hii kwa baadhi ya wanafunzi itapungua kama si kuisha kabisa, ni vyema pia wakajitokeza wadau wengine wakachangia kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwasaidia wanafunzi katika mkakati mzima wa kupunguza/kuwaondolea adha hii kama unavyo ona kwenye picha hii hapo juu.
-JIACHIE.

1 comment:

mangi said...

UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KATI YA MADHAMANA NA WADAU WA MRADI NDIYO SULUHISHO MAKINI.SASA TUWAOMBA NBC,NMB,BACLAYS,STANBIC,VODACOM,ZAIN,TIGO,ZANTEL,TBL,SERENGETI,PESPSI,COCACOLA NA WENGINE WOTE WACHANGIE MABASI YAO NA GHARAMA ZA UENDESHAJI IKIWA NI SEHEMU YA KURUDISHA FAIDA YAO KWA JAMII.

WATEMBELEAJI