Tuesday, June 8, 2010

PILIKA PILIKA NYINGI SANA...LAKINI TUPO PAMOJA DAIMA!

Wandugu, wadau wapendwa...ubize umenizidi kidogo, lakini tupo pamoja daima. Jana kutwa nzima kwangu ilikuwa ni safari tu. Niliondoka Cesena nikawasili Mjini Rome, baadae mjini London niliwasili usiku wa manane, lakini safari ilienda vizuri. Nitakuwepo hapa mpaka ijumaa, kusafisha macho kidogo. Maana sisi watu tunaotoka vijijini, mara moja moja si vibaya sana kusafisha macho. Wadau wapendwa wenye mapenzi mema walinialika hapa, nami nimeitikia wito wao, na vikazi vya hapa na pale vimenifanya niunganishe safari moja. Lakini libeneke la hapa kama kawaida tunandelea tuu....

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kila la kheri na asante kwa taarifa!!

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada Yasinta.

WATEMBELEAJI