Friday, October 8, 2010

JUMUIYA YA KIMATAIFA INAYOWAJIBU KULINDA HAKI ZA WATOTO.

JUMUIYA YA KIMATAIFA INAOWAJIBU WA KULINDA HAKI MSINGI ZA WATOTO WAKIMBIZI NA WAHAMIAJI.

-Mimi nasema; si haki sahihi kwa nchi za Ulaya kuwarudisha watoto wanaoingia Barani Ulaya, wakati mwingine bila ya kuwa na wazazi au walezi wao. Ni watoto ambao wameathirika kwa namna nyingi na wanatakiwa kutunzwa kwa namna ya pekee sanjari na kuzingatia haki zao msingi.

Msimamo huu umetolewa baada ya nchi kadhaa za Ulaya kuanza kuweka mikakati ya kuwarudisha watoto wanaokimbia hali ngumu ya maisha katika nchi zao kutokana na vita pamoja na uvunjifu wa haki msingi za binadamu, watoto wanaolazimishwa kwenda kupigana vita, wengine wametumbukizwa katika biashara haramu ya binadamu ya ukahaba.

Nchi za Ulaya ambazo zimeridhia haki msingi za watoto zilizotajwa na Umoja wa Mataifa, wanapaswa kulindwa na kusaidiwa kwani wameondolewa kutoka katika mazingira ya familia zao. Mtoto mwenyewe anapaswa kuangaliwa kama mhusika mkuu katika changamoto hizi na kwamba sheria ya uhamiaji kimataifa zinapaswa kulinda na kuheshimu haki msingi za watoto.

Watoto wakimbizi na wahamiaji, kimsingi kabla ya kuangalia masuala mengine ni watoto wenye haki na hadhi zao katika Jumuiya ya Kimataifa. Hivyo wanapaswa kuingizwa katika mipango ya Nchi husika, au kupelekwa katika nchi nyingine wanakoweza kupewa huduma msingi, kwa kulinda usalama wa maisha yao.

Watoto hao wakati mwingine wamesaidiwa na wazazi wao ili kuepuka hali ngumu katika nchi zao. Watoto hawa wanapaswa kwa hakika kusaidiwa kwa hali na mali. Jumuiya ya Kimataifa inawajibu na haki ya kulinda usalama wa watoto wanaokimbia kutoka katika nchi zao, ili wasije wakatumbukia katika mikono hatari ya watu wanaoweza kudhalilisha utu na heshima yao.

-WATOTO NI TAIFA LA KESHO, WANA HAKI YA KUPEWA MATUNZO VIZURI NA MALEZI BORA. JE WEWE USINGELITUNZWA VIZURI NA WAZAZI WAKO UNGEKUWA HIVYO ULIVYO SASA, UNGELIFIKIA HALI ULIYO NAYO SASA? TUTAFAKARI DAIMA NA KUWAPENDA WATOTO WOTE WA DUNIA HII, HATA KAMA SI WATOTO WETU WA KUWAZAA.

No comments:

WATEMBELEAJI