
Brrrrrrrrrrrr kanyonyonyooooooooo twendeeeeee.
Maneno ya Dada Yasinta haya, katika blog yake ya MAISHA NA MAFANIKIO.
-Nami nasema nilishawahi kusafiri sana na gari kama hili, pia nilikuwa mtundu sana wa kuyatengeneza (kuyaunda) Kijijini kwetu watoto wenzangu walikuwa wananitegemea sana katika utengenezaji, umenikumbusha mbali sana Dada Yasinta, tena majuzi tu tulikuwa tunaongelea maswala kama haya na rafiki yangu huko kijijini, tukisema utamaduni wa kuunda michezo kama hii unaenda unafifia tu! mpaka basi watoto wa siku hizi hata wa vijijini wanataka matoy tu kwa kucheza! Umenifurahisha sana tena sanaaaaa.......!!!!
Asante sana kwa picha hii nzuri Dada Yasinta!
No comments:
Post a Comment