Tuesday, February 15, 2011

AMSTERDAM...USO KWA USO NA MDAU MKUBWA WA BLOG HII.

Nikiwa safarini kurudi Italy kutoka nyumbani Tanzania, wakati tukitoka kwenye ndege tukiwa Amsterdam - Uholanzi. Mara nikasikia kwa nyuma yangu naitwa na mdau Dominic Mosha, nilishituka sana, na kumwuliza tunafahamiana? Alinijibu kuwa yeye huwa anafuatilia Blog hii, kwahiyo ananifahamu kwa kupitia blog ya KAZI YAKO NI JINA LAKO; kwa kuniona kwenye picha.
Kwakweli sikutegemea kabisa na nilikuwa na furaha sana tena sana....kwa kumfahamu mdau mkubwa wa Blog hii....kwa kufahamiana kwa njia hii. Ni furaha sana na ni moja ya upendo tulionao Watanzania.
Mdau Dominic alikuwa na safari yake ya ki kazi, hatukuweza kuongea vizuri zaidi maana tuligawanyika hapo Amsterdam, na muda wa ndege ulikuwa umewadia, lakini tuliweza kupiga picha ya pamoja hapo Airport. Tudumishe upendo daima wa kufahamiana na kujaliana. Asante sana mdau Dominic kwa upendo wako wa kujitokeza kwa kutaka kufahamiana vizuri.

-SALAMU SANA KWA MDAU MR: DOMINIC, TUPO PAMOJA DAIMA!

1 comment:

Unknown said...

Kazi yako jina lako... 10 years ago. hope you are keeping well Baraka.

WATEMBELEAJI