Monday, February 21, 2011

HII NILIIPENDA SANA..NILIKUTANA NAYO......

..........KWENYE MTANDAO FULANI, NAMI NAWALETEENI HAPA;



Uaminifu ni mbolea katika mapenzi. Na usaliti ni sumu kali sana, mbaya kabisa tena sana.
Wengi wapo kwenye uhusiano usiyo na afya sawasawa, kutokana na tamaa za pembeni; kwamba mmoja anashindwa kutosheka na aliyenaye, hivyo anakwenda kutafuta ''UROJO'' mtaa wa pili.

IPO TAFSIRI HII; Kumsaliti mwezi wako maana yake umemdharau, yaani umemuona ni mjinga wa mwisho kwenye mapenzi, ndio maana ukaamua kuitoa sadaka heshima yake.

JIULIZE; Yeye ndiye amezoea kukuona ukiwa katika hali zote, kesho unataka watu wengine wamtazame vipi ikiwa mwili wako umeutoa kwa wengine? Ina maana hauna uspesho tena kwake, anavyokujua na wengine ni hivyo hivyo.

FUMBA MACHO YAKO UTAFAKARI; Anakujua ukiwa hauna nguo, lakini hicho si kitu spesho tena kwani mtaa wa tatu yupo mwingine anayekujua vilivyo unapokuwa umesaula. Heshima ya kweli ipo wapi?

THAMINI UTU WAKO; Anayetembea bila nguo siku zote anaitwa kichaa, wewe fungu gani? Muungwana hawezi kabisa kufurahia kitendo cha viungo vyake vya siri kuonwa hovyo hovyo!

CHUKUA UKWELI HUU; Ukiona kwenzi wako anateseka baada ya kujua umemsaliti, maana yake anaumizwa na kumbukumbu ya yale ambayo huwa mnayafanya faragha, halafu anafikiri hicho hicho ndicho ulichokipeleka nje!

KINACHO MTESA; Ule muonekano wako eneo la tukio, vitendo vyako kwake ni ile ladha ambayo huwa anaipata kwako, halafu unajiona yeye si mali kitu tena kwasababu vyote ummempa mwingine. Heshima yake ipo wapi?

TAMBUA; Mapenzi ni kitu maalum, ya kwako na mwenzako...yabaki kuwa yenu tu! ndiyo maana mkaitwa wasiri. Wewe utakuwa na wasiri wangapi ikiwa unashindwa kutulizana kwa mmoja?? Unapata siri gani ikiwa siri zako za chumbani wanazijua watu 20?

-Kusaliti penzi ni kitu kibaya sana tena sanaaa.....katika hii Dunia ya sasa ambayo walimwengu wanapambana na maradhi mbalimbali yanayotokana na kutokuwa waaminifu katika mapenzi. Hupaswi kuwa na tamaa hasa pale umpatapo yule anaye kupenda kwa moyo wake wote, yupo tayari hata kufa kwaajili yako.
Hupaswi kuwa na tamaa kwa kuhisi kuwa utapata vitamu zaidi pembeni. Hivi vitamu vitakuua ndugu yangu, acha kutanga tanga kila kukicha!

-MPENDE AKUPENDAE...ASIYE KUPENDA ACHANA NAE KABISA TENA MAPEMA KABISA!










No comments:

WATEMBELEAJI