Nami nimezitumaini fadhili zako; moyo wangu na uufurahie wokovu wako. Naam!!! nimwimbie Bwana, kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.
Ee nafsi yangu umimidi Bwana, naam! vyote vilivyo ndani yangu, vilihimidi jina lako takatifu. Ee nafsi yangu umhimidi Bwana, wala usizisahau fadhili zake zote.
Akusamehe maovu yako yote, akuponye magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na neema. Bwana amejaa huruma na neema, haoni hasira upesi ni mwingi wa fadhili, wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.
Ee Mungu Mwenyezi, tunakuomba utujalie kuwaza daima mambo yanayofaa na kutimiza kwa maneno na matendo yanayokupendeza.
1 comment:
ni jumapili ya nane kaka baraka. Jumapili njema nawe pia:-)
Post a Comment