Tuesday, February 8, 2011

MARAFIKI WA ITALY NA UBISHI KUWA TZ HAKUNA BARIDI!

Marafiki wa Kiitaly Walter na mkewe Alda...walishangaa sana kukutana na baridi ya kufa mtu huko Makalala - Mafinga, mwaka jana walipo kwenda na mimi kutembelea kituo cha watoto yatima cha Makalala - Mafinga, na Tanzania kwa ujumla.
Wakati tunajiandaa na safari tukiwa bado hukuhuku, niliwaambia kuwa tayarisheni na masweta maana Makalala na Ngorongoro kuna baridi, walinibishia sana kuwa Afrika kuna baridi??? haiwezekai kabisa. Mimi niliwaambia sawa lakini mimi nimewaambieni, habari ndo hiyo! Tulianza kwenda Ngorongoro huko ikawa balaa mpaka tukatafuta masweta kwa shida pale Karatu, tukanunua hayo walio nayo hapo kwenye picha. Kufika Makalala -Mafinga hapo ndipo ilikuwa balaa zaidi, mpaka leo hii wanahadisia sana kuhusu swala hilo. Wazungu wengi sana ukiwaambia hata kwetu kuna baridi sana sio ya barafu, lakini ipo, huwa wanabisha sana...wanakataa kabisa, wao wanaamini kuwa sisi tunakuwa weusi kwaajili ya jua kali daima linatuunguza ndio maana tunakuwa weusi, kama mimi ndio usiseme huwa wananitania kwa kusema umeunguzwa kweli kweli na jua, kwa weusi wangu nilio nao.

No comments:

WATEMBELEAJI