Friday, March 25, 2011

DRAFT KULICHEZA NI TAMU SANA...ULIJUE LAKINI!

Napenda sana kucheza draft nikiwa nyumbani TZ, pia na story za hapo kwenye draft ni vicheko kwenda mbele. Waafrika tuna raha sana mambo kama haya Majuu hakuna, na hawana muda kabisa. Lakini mimi naona inasaidia sana wakati mwingine, watu wanafahamiana kwenye mambo kama haya na wanakuwa kama ndugu kabisa. Pia kupumzisha kidogo akili kwa kufurahi na wenzako si jambo dogo hili. Ndio maana watu Ulaya wanachanganyikiwa kwa vitu vidogo sana, maana hupati mtu hata wa kukuuliza vitu ndugu yangu una matatizo gani?

Hapa kwenye picha ni kijiwe cha Chalinze, kwa rafiki yangu Shebi. Picha kutoka kwa Mjengwa.

No comments:

WATEMBELEAJI