Monday, March 21, 2011

HAYAWI HAYAWI.....HATIMAYE YAMEKUWA!

KIBURI, FAHARI NA UTUKUFU WA GADDAFI VIMEFIKIA UKINGONI.



Hakika Dunia hii hakuna anayeweza kutamba milele, kama ni ubabe mtu anaweza kuwa nao kwa muda tu!Hivi ni nani aliyewahi kufikiria au hata kwa kuota tu......kwamba Gaddafi atakuja kung'oka madarakani kwa nguvu bila ridhaa yake? Kwa jinsi hali ilivyo, Gaddafi atafikishwa katika mahakama ya Kimataifa nchini Uholanzi, ndani ya muda mfupi ujao. Mataifa yenye nguvu za Kijeshi Duniani yapo katika kumsaka sasa. Muda mfupi ujao tutasikia mazito kutoka Libya. Mataifa hayo ni; Marekani, Ufaransa, Uingereza, Denmark, Canada...nk.

Labda hili linaweza kuwa fundisho kwa viongozi wengine wa Kiafrika wanaopenda sana kung'ang'ania madaraka daima. Tuzidi kuomba Mungu yasitokee na kwetu haya.

No comments:

WATEMBELEAJI