
Namkumbuka sana huyu jamaa na vituko vyake....wakati nikiwa shule ya msingi moja ya wimbo wa mchakamchaka wa kila siku tulikuwa tukiimba hivi;Idi Amini...akifa mimi siwezi kulia, nitamtupa kagera awe chakula cha mamba!
Hii yote ilikuwa ni kwasababu ya ubabe wake, alio kuwa nao kwa watu wake.
- Moja ya ndoto zake Idi Amini...aliitimiza, ni hii ya kubebwa na wazungu. Alisema nikiichukua nchi hii tu! ( kwa utawala wa kuwa Rais) lazima wazungu wanibebe, alisema; wao waliwatumikisha wazee wetu bila aibu, sasa zamu yao. Duuhhh....!!!! Jamaa huyu kweli alikuwa kiboko, mbabe balaa, kwa vituko alivyokuwa akivifanya mpaka basi! Baada ya kusoma historia ya vituko vyake alivyokuwa akivifanya, kuna moja lilinichekesha sana ni hili; kumwandikia barua ya kimapenzi Malkia wa Uingereza, na kumwambia mambo kibao na pia anataka kumwoa kabisa.
1 comment:
Alikuwa kiboko ya wazungu.
Post a Comment