Hapa ni maeneo ya Tanangozi kabla hujafika Mafinga ukielekea katika Mbeya road, tulikuta ajali ndo imetokea tu na kushuhudia watu wakitolewa kwenye Daladala...ambapo watu 9 walikufa papo hapo na wengine kujeruhiwa sana. Ajali ilikuwa inatisha sana, lori moja liliivamia Coaster ambayo ilikuwa imepaki pembeni mwa barabara ikishusha watu, lori hilo lilikosa mwelekeo..likaigonga daladala hiyo na kwenda kutumbukia kwenye mfereji. Kijijini Tanangozi ilikuwa huzuni sana na majonzi kwa wingi. Haya ndo mambo ya barabarani, ukiwa unasafiri...kwa Tanzania lazima ukutane nayo kwa wingi sana kila uendepo.
No comments:
Post a Comment