.......WA KIMAABARA. HAYA NI MAONI YA MWENZETU ALIYE ARUSHA: ANASEMA;
Hapa Arusha kila Hospitali imepokea watu wagonjwa wa Presha, Kisukari, Pumu nk.....ambao walikwenda Loliondo kutibiwa maradhi hayo na baada ya kupata nafuu ( PSYCHOLOGICAL) kwa kama wiki mbili tu! wameanza kuumwa (SERIOUSLY) na kurudia dawa zao za Hospitali tena.
Pili, mimi nikiwa mfanyakazi wa maabara ya Hospitali ya MT.Meru, sijaona hata mgonjwa mmoja wa Ukimwi aliyepata ''SEROCONVERSION'' yaani kurudi ''SERONEGATIVE FROM SEROPOSITIVE STATUS''. Kinachosikitisha ni kuwa kuna watu hawataki kabisa kusikia yanayosemwa na Madaktari na wafanyakazi wa Hospitali mbalimbali hapa Arusha ambao kila siku tuna-deal na watu wanaozidiwa baada ya kwenda Loliondo.
Mbaya zaidi kuna Magazeti, Tv na Redio hayataki kabisa kusikia ukweli wa majanga yaliyo wafikia watu waliokwenda huko. Ajabu pia ni kuwa kuna watu ambao ukitaka kuwaeleza ukweli wanakuona wewe hufai, wale walioenda huko....wanakuona wewe ni mpagani usiyemwamini Mungu. Naomba sana waandishi wa Habari wawe Proactive katika kutafuta ukweli na si kutegemea mass hysteria iliyowakumba maelfu ya watu wanaotafuta miujiza kwa nguvu.
- Kutoka kwa Mkuu Maggid Mjengwa.
No comments:
Post a Comment