TAREHE 8 MARCHI, 2011: MIAKA MIA MOJA YA MIKAKATI YA KUDUMISHA USAWA NA MAENDELEO YA WANAWAKE.......... HAPPY WOMAN'S DAY!
Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha siku ya wanawake Kimataifa kila ifikapo tarehe 8 Marchi, lakini kwa mwaka huu haya ni maadhimisho maalum kwani Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Karne moja tangu mikakati ya kudumisha usawa pamoja na kuwawezesha wanawake ilipoanzishwa.
Kumekwepo na mfanikio makubwa katika mchakato wa kuwawezesha wanawake katika medani mbalimbali za maisha. Lakini bado wanawake wanaonekana kuwa ni raia wa daraja la pili. Maadhimisho ya siku ya wanawake Kimataifa yanaendelea kukazia umuhimu wa fursa sawa katika elimu, mafunzo pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya habari, ili kuboresha ustawi na maisha ya familia zao. Kuondokana na umaskini wa kipato pamoja na kusimama kidete kulina na kutetea misingi ya haki na Amani.
Katika uringo wa siasa wanawake wengi wanaendelea kucharuka kwa kushika nafasi za juu katika Bunge, lakini bado idadi ndogo sana ya wanawake ambao kwa sasa ni wakuu wa nchi. Kuna haja ya kuendelea kuwashirikisha katika utungaji na uteelezaji wa maamuzi mbalimbali yanayofanywa katika sekta ya uchumi na maendeleo ya viwanda.
- HAPPY WOMAN'S DAY!
1 comment:
Hongera akina mama wote kwa siku hii. Tuzidishe ushirikiano na upendo.
Post a Comment