Sunday, March 27, 2011

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII YA 3 YA KWARESIMA!

SALA HII NAIPENDA SANA, NILISHAWAHI KUIANDIKA (KUIWEKA) HAPA. LAKINI NAOMBA NIIRUDIE TENA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KWARESIMA, SALA NI HII;



Nia yangu naileta kwako Bwana Mungu wangu, nakuomba sana Bwana unisikie...ninalia kwa uchungu. Nakomba uipokee sala yangu, sikiliza na sauti ya kilio changu. Ninajua Bwana siku zote wewe hupatikani kwenye ghasia, ninajua siku zote hupatikani kwenye vurugu.
Bwana unijalie utulivu wa moyoni na unipe nguvu, shusha roho wako anipe faraja. Bwana niongoze ili nitimize nia yangu ya kuwa mtumishi mwema.

Ee Bwana upo wapi mimi ninakutafuta, nitazame kwa huruma nateseka Mungu wangu, nakuomba ipokee sala yangu sikilia na sauti yakilio changu. Ninajua kabisa Bwana siku zote wewe hupatikani kweye ghasia, ninajua siku zote hupatikani kwenye vurugu.

Hata kama nipo.... kama takataka kwa watu, mbele yako mimi ni thamani kubwa sana siku zote. Nakuomba sana ipokee sala yangu na sikiliza sauti ya kilio changu.
Ee Bwana Mungu wangu, nijalie nikabili njia zangu, nimshinde huyu mwovu shetani hanifai. Nakuomba sana ee Mungu wangu ipokee sala yangu na sikiliza sauti ya kilio changu.

1 comment:

Anonymous said...

Kuna wimbo unaimbwa hivihivi kama unao plz naomba U upload

WATEMBELEAJI