Sunday, March 27, 2011

MDAU MMOJA ANASEMA KUHUSU;..KILI AWARDS TANZANIA.

KILI AWARDS....WATANZANIA NA UMASKINI WA KUCHANGUA.

Mpoki akiwakilisha, kwa kuwashukuru wapenzi wake.
MSANII MPOKI AKITOA SHUKRANI ZAKE KWA MASHABIKI WAKE, WALIOMWEZESHA KUPATA TUZO YA WIMBO BORA WA ASILI TANZANIA.


Nilikutana na hii habari sehemu fulani ya mdau mmoja akichangia mawazo na maoni yake, kwa kusema;


Sitaki kuamini kama ni Watanzania ndio wamemchagua mwimbaji bora kwa wimbo wa Asili ya Tanzania kuwa ni Mpoki, na kibao chake cha SHANGAZI....katika kinyang'anyiro cha tuzo hiyo, iliyowashirikisha Wasanii wengine kama Mrisho Mpoto na kibao cha ADELA, lakini kura za Watanzania zilimwangukia Mpoki. Ikiwa kama Watanzania wa leo tunachagua nyimbo zenye mashairi ya; SHANGAZI UNA NYETI KULIKO HIZI TULIZONAZO, NYOKA HANA KIUNO NDO MAANA HAVAI SHANGA.....kama anavyoimba Mpoki, na kuacha nyimbo zenye mashairi ya kutufundisha na kuonya,,,basi tumekwisha kabisa!


- Mdau anawakilisha.



1 comment:

ANGELA said...

HATA BINAFSI KWA KWELI NILISHANGAA SANA HAKUSTAHILI KUPATA TUZO HII YAANI PALE SITTING ROOM WOTE HATUKUAMNI TULIBAKI MIDOMO WAZI BINAFSI IMENIPA WALAKINI KWENYE UCHAGUZI WAO.

WATEMBELEAJI