Monday, March 21, 2011

MISALABA YARUHUSIWA KUTUMIKA MASHULENI ULAYA!

Mahakama ya haki za binaadamu Ulaya imesema kuwa misalaba yenye sanamu ya Yesu inaruhusiwa kuwepo katika madarasa ya shule za umma.
Uamzi huo ulitolewa na mahakama hiyo Strasbourg, unazihusisha nchi zote 47 ambazo ni wanachama wa Baraza la Ulaya, chombo kinacho simamia haki za binaadamu Barani humo.
Novemba mwaka 2009 mahakama ilisema kuwa misalaba yenye sanamu ya Yesu inaweza ikawa usumbufu kwa wanafunzi ambao sio Wakristu na wale wanaomkana Mungu, hivyo ilisitisha kuwepo kwa misalaba mashuleni. Kwasasa ni ruksa!

No comments:

WATEMBELEAJI