Friday, March 25, 2011

TANZANIA KILA SIKU AJALI AJALI.....MPAKA LINI?

AJALI YA BASI LA OSAKA MKOANI MOROGORO. Basi la Osaka likiwa limepinduka baada ya kugongana na Fuso Kijijini Maseyu, barabara ya Morogoro - Iringa. Katika ajali hii watu 27 wamejeruhiwa.
Lori la mizigo aina ya Fuso lililogongana na basi hilo.
-Picha na Juma Mtanda.
Hivi hizi ajali Tanzania za kila siku zinazouwa sana wapendwa wetu, tumeshindwa kabisa kuzidhibiti kweli? Yaani kila kukicha ajali ajali!!!! Na bado tunaona kila siku magari mabovu yapo tu barabarani bila wasiwasi wowote, yameshehena mizigo kupita kiasi, pia kasi yanavyokimbia barabarani balaa....bila kufuata sheria za barabarani. Hivi kweli kabisa tumeshindwa kabisa kudhibiti swala hili na kuacha watu, ndugu zetu wakiendelea kufa na ajali za kizembe kizembe? Jamani wahusika chonde chonde fuatilieni kwa makini sana swala hili....la sivyo mtaendelea kutumaliza kila kukicha na ajali za kizembe tu!

No comments:

WATEMBELEAJI