Thursday, March 24, 2011

UKATOLIKI HATA UWE NANI...LAZIMA UBUSU PETE YA ASKOFU!

Kanisa Katoliki lina mambo mbalimbali ya kikanisa na sheria zake...kama yalivyo madhehebu mengine na dini zingine na sheria zao.
Hapa kwenye picha Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda, akibusu pete ya Askofu Kilaini wa Jimbo la Bukoba. Waziri Mkuu ni Mkatoliki...na sheria ya Kanisa hilo kuwa ukiwa unasalimiana na Askofu au Papa ni vizuri ukabusu pete aliyovaa....maana pete hiyo inawakilisha heshima ya kanisa zima, na utiifu kwa viongozi wa kanisa hilo.

Hii picha niliipenda sana...pamoja kuwa Mh.Pinda ni mkuu wa nchi, lakini inaonyesha wazi kuwa ni mwanadini hasa na anaheshimu na kutii sheria za kanisa, pia Mh.Pinda ana kumbukumbu kama hiyo, maana mimi binafsi mara nyingi huwa inanitokea nasahau kabisa kubusu pete hiyo wakati nikisalimiana na maaskofu, huwa nawapa mkono tu maaskofu, baadae kabisa nakumbuka nilipaswa kubusu pete. Hongera sana kwa Mh.Mizengo Pinda kwa utii huu kwa Yesu Kristu na kwa kanisa kwa ujumla.

No comments:

WATEMBELEAJI