Tuesday, March 1, 2011

WATANO WAFA KWA AJALI.....DODOMA!



Watu watano wamekufa papo hapo na wengine 34 kujeruhiwa, katika ajali iliyo yahusisha magari mawili ya abiria, yanayofanya safari zake kati ya Kahama na Dar es salaam, na jingine Itigi - Dodoma.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa sita mchana katika eneo la Mbwanga karibu na mizani ya Tanroad, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Ajali hiyo ilihusisha Basi la Kampuni ya Ally's lenye namba T 312 AUU, lililokuwa likitokea Kahama kuelekea Dar es salaam, ambalo liligongana na Gari aina ya Coaster lenye namba T 896 BGH, ambalo lilikuwa likitokea Dodoma kuelekea Itigi, Wilayani Manyoni.

No comments:

WATEMBELEAJI